Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni walinzi ambao mpaka sasa majina yao hayajafahamika wameuwawa na watu wasio julikana usiku wa kuamkia Disemba 13 katika kijiji cha Busanda Kata ya Busanda Wilaya na Mkoa Wa Geita.
Mmoja wa Askari Polisi kutoka jeshi la polisi Mkoa wa Geita Michael Masume amekemea vikali matukio ya ukatili hasa mauaji ambapo amesema vitendo hivyo vinagharimu maisha ya watu wasio na hatia na kupekea familia zao kubaki kukosa wasaidizi.
Zotekali blog bado inaendelea na jitihada za kumtafuta kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa geita ili kuweza kujua undani wa tukio hilo pamoja na hatua ambazo zimeshafikia mpaka hivi sasa.
0 Comments