Wateja zaidi ya 500 wa wa Benki ya CRDB wamefanikiwa kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha ,magari, compyuta ,simu janja na hiyo ni kitu kikubwa na muhimu kwa benki hiyo na wateja wake kwa ujumla.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa kitengo cha wateja na Biashara CRDB,Steven Adill wakati wa hafla ya kukabidhi gari iliyofanyika katika benki ya CRDB tawi la Usa River jijini Arusha.
Adill alisema kuwa benki ya CRDB ilitenga kiasi cha Sh milioni 350 kwa ajili ya kampeni hiyo iliyozinduliwa februali 14 mwaka huu katika mji wa Mbagala Jijini Dar-es-salaam.
Pamoja na hayo Benki ya CRDB imekabidhi gari jipya aina ya Vanguard lenye thamani ya Milioni 30 kwa mshindi wa jumla Dk Bakati Zuberi akitokea mkoanu Arusha,aliyeshinda kupitia kampeni maalumu ya Benki SimBanking kupitia simu za mkononi.
Kwa upande wake mshindi wa gari hilo,Dkt Bakari Zuberi aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma hiyo ambayo imempa urahisi wa kufanya malipo mbalimbali na kumwondolea gharama ya kwenda benki kwa ajili ya huduma za kifedha.
Aliwashauri wateja wa benki hiyo kujiunga na huduma ya SimBanking na kuacha kuogopa makato kwani gharama za kufuata huduma za kifedha katika benki ni kubwa kuliko kutumia malipo kupitia SimBanking.
“Baada ya kushinda watu wengi sana walinipigia simu kutaka kujua nimeshindaje, ila mimi nataka niwaambie siri ya ushindi wangu nilikuwa natumia sana SimBanking na asilimia 90 ya malipo yangu yote natumia SimBanking “..
0 Comments