Wananchi Hanang waomba dawa ziongezwe

 


MANYARA: Wananchi wa Kijiji cha Jorodom wamevutiwa na jitihada za Serikali zinazoendelea za uelimishaji wa jinsi ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko pamoja na usambazaji wa dawa za kutibu maji katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.

Wakizungumza baadhi ya wananchi wakati wakiendelea kupata elimu hiyo wameomba dawa za kutibu maji ziongezwe ili kukidhi mahitaji.


Mwenyekiti Kijiji cha Jarodom amesema hatua ya serikali kusambaza mabango ya kuelimisha kuhusu kuzingatia kanuni za afya kujikinga na magonjwa pamoja na usambazaji wa mabango ni nzuri katika kuwajali wananchi wake.

“Hii elimu ni nzuri sana maana maana inatupa mwongozo tufanye nini pia kitendo cha kutibu maji mnajali usalama wetu tunataka vidonge zaidi na zaidi “amesema mmoja wa wananchi hao.


Ikumbukwe kuwa Jorodom ni kijiji cha kwanza kuathiriwa na maji ya mafuriko yaliyoambatana na maporoko ya tope ,magogo na mawe hali iliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya maji, nyumba na vitu mbalimbali.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE