Neil Hagari, Msemaji wa Jeshi la utawala haramu wa Israel alitangaza jana Jumamosi kuhusu kuangamizwa askari 5 wa utawala huo na kujeruhiwa wengine 5 katika mapigano ya nchi kavu kati ya askari hao vamizi na Wanamuqawama wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa IRNA, Hagari pia ameongeza kuwa, idadi ya askari wa Kizayuni walioangamizwa katika mashambuli ya nchi kavu huko Gaza imefika 144.
Kwa mujibu wa Ripoti hiyo idadi ya askari jeshi wa utawala huo ghasibu walioangamizwa tokea ilipoanza operesheni ya Kimbunga cha Al aqsa hadi sasa ni 477 ambapo 144 wameangamia tangu kuanza operesheni ya nchi kavu huko Gaza.
Jeshi vamizi la Kizayuni pia limekiri kwamba askari wake 42 wamejeruhiwa katika mapigano makali kati yao na wanamapambano shujaa wa Kipalestina katika masaa 24 yaliyopita katika Ukanda wa Gaza.
Siku ya Jumamosi, tarehe 7 Oktoba 2023, makundi ya muqawama ya Palestina yalianzisha operesheni ya kushtukiza ya Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Gaza kusini mwa Palestina dhidi ya maeneo ya utawala unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu, ili kulipiza kisasi na kufidia fedhehe ya kipigo hicho kikali cha makundi ya Muqawama, ambapo umekuwa ukiua kwa umati wakazi wa ukanda huo na vilevile kufunga vivuko vyote vinavyotumika kuingiza bidhaa na misaada ya dharura katika ukanda huo.
0 Comments