Usimtafutie makosa

 Hapa dunıanı hakuna mtu yeyote ambaye anazo sifa zote zılızokamılıka na asiyekuwa na makosa. Watu wengine wanaweza kuwa wanene sana au wembamba sana. Wenye midomo mikubwa, pua kubwa au meno makubwa. Wengine wanakuwa wachafu, hawana adabu, wenye haya, fidhuli, wenye kuvunjika moyo, hasira, wivu au wachoyo. Wanawake wengine si wapishi wazuri au mwanamke mwenye kipaji. Watu wengine wanaweza kuwa walaji sana au kutumia kwa fujo. Kwa ufupi, hakuna mtu ambaye hana upungufu na kasoro, na hakuna mtu yeyote hapa duniani anayeweza kuchukuliwa kama kiumbe aliyekamilika.


Kwa kawaida, mwanaume, kabla ya kuoa hudhani kwamba atakayemuoa awe hana dosari yoyote. Hawaangalii ukweli huu kwamba hakuna kiumbe afanana na malaika hapa ulimwenguni. Wanaume hawa, mara waoapo huwaona wake zao waliodhani wakamilifu, si wakamilifu na hivyo huanza kuonesha mapungufu yao. Hudiriki kuona kuwa ndoa zao hazikufanikiwa na kujiona kuwa wana ‘bahati mbaya.’ Wanaume hawa hulalamika kila mara na hawaachi kulalamikia hata dosari ndogo za wake zao.

Wanaume wengine hukuza dosari sana kiasi kwamba kila mara huziona kubwa kama milima Kilimanjaro. Mara kwa mara huzitaja dosari hizo kwa wake zao na kuwadhalilisha. Pengine huzitaja hata mbele ya marafiki na ndugu. Matokeo yake msingi wa maisha yao ya ndoa huanza kutetereka. Mwanamke hufadhaika na hupoteza shauku kwa mume wake na familiayake. Ataona kuwa sasa hakuna mantiki yoyote kufanya kazi kwenye nyumba ya mtu ambaye muda wote humshutumu. Inawezekana akalipiza kisasi.

Mwanaume atamwambia mkewe: “Tazama pua yako ilivyo kubwa, mbaya kweli kweli!” Na mwanamke atajibu: “Si mbaya kama uso wako mbayana kiwiliwili chako kilicho kwenda kombo!”

Halafu mwanaume atasema: “Meno yako yananuka harufu mbaya! Na mwanamke anajibu: “Funga domo lako kubwa.” Na kadhalika.

Kuendelea kwa mazungumzo haya hufungua mlango wa shutuma na kuigeuza nyumba kuwa uwanja wa vita ambamo wanandoa hutukanana na kushushiana hadhi. Wakiendelea kuishi namna hii, hawatafurahia maisha yao tena hata kidogo, kwa sababu nyumba isiyokuwa na mapenzi ya familia na uaminifu, si mahali pa faraja.

Aidha, mwanaume anayejihisi kwamba yeye hana bahati na ndoa yake imeshindikana, na mwanamke ambaye hudhalilishwa wakati wote, wote wawili wanaweza kupata maradhi ya kiakili na mengineyo.

Ugomvi wao ukizidi kuongezeka basi kila mara huwa kunakuwepo uwezekano wa hatari ya kutalikiana au kutengana. Kutalikiana ni hatua isiyosaidia sana kwa pande zote zinazohusika, haswa kama wapo watoto katika familia. Jamii huwa haiwapendi kabisa mtalaka mwanaume au mwanamke. Zaidi ya hayo kutalikiana ni hatua inayosababisha hasara ya kiuchumi kwa mwanaume; ambayo si rahisi kurekebishwa hasa pale mtalaka anapotaka kuoa tena, kwani pia atahitaji kutumia fedha tena kwenye ndoa yake ya pili. Zaidi ya hayo, hakuna uhakika wa mtalaka kupata mwanaume ambaye atamridhisha kufuatana na matumaini yake.

Kufunga ndoa mara ya pili haitakuwa rahisi kwa sababu ya historia yake. Hata kama mwanamume atapata mwanamke mwingine, bila shaka atakuwa na mapungufu fulani pia. Anaweza hata akawa mbaya zaidi kuliko mke wake wa kwanza. Atakuwa hana budi kumvumilia. Hii ni kwa sababu wanaume wengine wanayo majivuno makubwa na hawataki kukubali dosari zao.

Ni mara chache sana utamuona mwanaume ambaye ameridhika kabisa na ndoa yake ya pili. Imewahi kutokea kwamba baadhi ya wanaume hurudi kwa wake zao wa mwanzo.

Kaka yangu! Kwa nini umwangalie mke wako kwa lengo la kutaka kugundua dosari zake; na kwa nini utilie maanani sana kuhusu mapungufu madogo? Kwa nini uyakuze sana makosa yake kiasi cha kujisababishia mateso wewe na familia yako?

Umepata kumuona mwanamke asiye na dosari kabisa? Wewe mwenywe ni mbora kwa kiwango gani? Kwa nini uzipe nafasi dosari ndogo ndogo zitakazohatarisha ndoa yenu?

Tambua kuwa ukimuangalia mkeo kwa jicho lenye mantiki na haki, utagundua mambo mengi mazuri kuhusu yeye. Ukiangalia zaidi utagundua kuwa mazuri yake yanazidi dosari zake.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE