Tanzania yatoswa waamuzi AFCON


 CAIRO: Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza majina 68 ya waamuzi watakaosimamia michezo ya Michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika mwakani nchini Ivory Coast.

Katika waamuzi hao 68 waliotangazwa 26 ni waamuzi wa kati, 30 ni waamuzi wasaidizi wakati waamuzi 12 ni wa VAR.

Kwenye orodha hIyo hakuna jina la mwamuzi kutoka Tanzania huku majirani Kenya wakifanikiwa kupeleka waamuzi katika michuano hiyo mikubwa Afrika.

Mwamuzi, Salima Mukansanga kutoka Rwanda ambaye kwasiku za hivi karibuni amejitambulisha katika ulimwengu wa kandanda kutokana na uhodari wake wa kuzimudu vyema sheria za mpira wa miguu, amepenya tena katika michuano mingine mikubwa baada ya kutamba katika kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar.

Ikumbukwe Michuano ya Afcon inatarijiwa kuanza January 13 hadi February 11, 2024 nchini Ivory Coast na Tanzania ni miongoni mwa mataifa 24 yatakayoshiriki mitanange hiyo nchini Ivory Coast.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE