Singida Fountain Gate (SFG) imeachana na kocha mkuu Ricardo Ferreira aliyedumu kwa miezi miwili tangu Oktoba 15.
Ferreira ameeleza mambo yalianza kuonekana mabaya Desemba 21 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold walikopoteza kwa bao 1-0.
“Ni kweli nimesitishiwa mkataba na Singida na nilianza kupewa taarifa kupitia wakala wangu aliyeambiwa na rais wa klabu, Japhet Makau. Hivyo kwa sasa najiandaa kurudi Brazil,” alisema.
Ferreira aliyesaini mkataba hadi Julai mwakani ameiongoza Singida katika michezo tisa ya ligi akishinda minne, sare tatu na kupoteza miwili akiiacha nafasi ya tano na pointi 20.
Mbrazili huyo anakuwa kocha wa tatu kuondoka baada ya Mholanzi Hans Van de Pluijm aliyeiongoza kufuzu hatua ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3 dhidi ya JKU baada ya awali kushinda 4-1 huku Ligi Kuu akiiongoza kwa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ulioisha kwa suluhu.
0 Comments