Uongozi wa Simba SC umesema umetenga fungu la kutosha kwa ajili ya kufanya usajili wa nguvu kwenye dirisha dogo ambalo linmefunguliwa wiki iliyopita.
Katika dirisha dogo Simba SC imepanga kusajili wachezaji wanne wanaomudu nafasi ya Ushambuliaji, Kiungo Mshambuliaji, Winga na Beki wa Kushoto.
Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Imani Kajula amesema wamemruhusu Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha sababu ndiye anayehusika moja kwa moja na usajili.
“Kocha ametuletea mapendekezo yake ametuambia mapungufu yaliyopo kwenye kikosi na aina na idadi ya wachezaji anaohitaji kusajili kwenye dirisha dogo na uongozi umemkubalia na kumtengea fungu la kutosha kwa ajili ya kupata saini za hao wachezaji,” amesema Kajula.
Amesema mikakati ya uongozi ni kuhakikisha wanamtimizia Benchikha mahitaji yake muhimu ili kuiboresha timu hiyo iweze kurudisha heshima iliyopotea katika michuano ya ndani na kufika Nusu Fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Amesema kamati yao ya usajili ipo karibu na Benchi la Ufundi kuhakikisha wanawapata wachezaji ambao kocha anawahitaji ili kukiimarisha kikosi chake ambacho kwa sasa kipo nafasi ya tatu kwenye Msimamo wa Ligi Kuu na kinapambana kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 Comments