Maisha yana option 2 tu, Kutumwa au Kujituma. Kila mtu ana uhuru wa kuchagua njia yake. sambaza Iwafikie Wengi! 1. Chagua hustle zako vizuri. Usiwe mtu wa kufanya vitu na kuishia njiani. Unahitaji kufanya mambo unayoweza kuwekeza muda wako kwa muda mrefu zaidi. Usifanye kisa fulani anafanya na anapata pesa. Chagua hustle unazoweza kuwekeza time hata kama matunda yako mbele zaidi. 2. Acha kupoteza muda wako kufanya mambo yasioyo na maana. Wekeza kwako. Punguza kupati. Wekeza kwenye maarifa. Punguza tamaa na mapenzi. Focus kwenye yake tu yanakufanya wa thamani zaidi. 3. Funga mdomo, usikilize na kupiga kazi. Maneno kidogo, vitendo vingi. Unapokutanana watu wanajua kuliko wewe. Funga mdomo. Sikiliza na ujifunze. Usijifanye mjuaji kwenye kila kitu. Unahitaji kijifunza na kufata njia zilizothibitika. 4. Epuka kuwa kwenye circle ya walalamikaji. Marafiki zako ni wastani wa wewe ulivyo. Tunao wana, tumetoka mbali. Ni kweli. Kama hawakuongezei kitu kwenye hustle zako, Fikiria mara 2. Unahitaji kuzungukwa na watu, Watu wanaokupush na kukushika mkono. 5. Usikubali hofu na woga vikuzidie. Kila mtu ana hofu, lakini reactions ndo tofauti. Huwezi kumaliza hofu, itakupiga tu. Jambo la msingi nikuwa mgumu na Kufanya unachopaswa kufanya bila kujali hofu. Just do it anyway. 6. Usipoteze muda kumfurahisha kila mtu. Huwezi. Utapoteza muda tu. Focus kwenye mishe zako. Fanya yaliyo ya muhimu kwako. Unapotenda wema, kuwa genuine. Usiwe na matarajio makubwa nje. 7. Kataa raha nyepesi na shortcuts. Hakuna growth inakuja kwa lelemama. Unahitaji kujikataa ili kuwa yule unataka. Unataka kuwa bora, wekeza kwako. Unataka kuwa wa kaiwada, lala magetoni 24/7.
0 Comments