Niliposikia kuhusu haya (mafuriko) nilimtafuta gavana na akahakikisha kwamba tumefika hapa salama na kila kitu kinakwenda kama ilivyopangwa," Odero alisema.
Mmiliki wa Kanisa la New Life Church Mchungaji Ezekiel Odero siku ya Krismasi alitembelea kaunti ya Tana River na kutoa Ksh10 milioni na vyakula kwa waathiriwa wa mvua ya El Nino hivi majuzi.
Kwa usaidizi wa serikali ya kaunti ya Tana River na Gavana Dhadho Godhana, mhubiri huyo mwenye utata alisema mchango huo ulitoka kwa kanisa lake kama sehemu ya ahadi aliyotoa kwa wakazi wa Tana River.
"Niliposikia kuhusu haya (mafuriko) nilimtafuta gavana na akahakikisha kwamba tumefika hapa salama na kila kitu kinakwenda kama ilivyopangwa," Odero alisema.
Akidokeza kuhusu kukumbana na vikwazo katika dhamira yake ya kuwasaidia walioathirika, Odero alisema uongozi wa Tana River ulikubali msaada huo na wananchi walinufaika na michango hiyo.
Mhubiri huyo pia alitetea serikali ya kaunti na ile ya kitaifa dhidi ya lawama, akisema walipopanga bajeti zao hakukuwa na utabiri wa mvua za El Nino.
"Ukweli usemwe, wakati mwingine tunalaumu serikali za kaunti na kitaifa kwa mafuriko lakini tayari walikuwa wamefanya bajeti zao kabla ya mafuriko kuja," Odero aliongeza.
Alisema serikali hizo mbili zimejaribu kufanya kila ziwezalo kwa waathiriwa wa mafuriko hayo na inapaswa kupongezwa kwa hilo.
Muhubiri huyo aligonga vichwa vya habari baada ya kukamatwa na kanisa lake kufungwa, kufuatia kuhusishwa na kanisa la Mackenzie ambaye yuko korokoroni kwa kuwadanganya waumini wake kukoma kula hadi kufa.
0 Comments