Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania Christina Shusho amewasili Nairobi kabla ya tamasha lake ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu.
Tamasha la Shusho limepangwa kufanyika Disemba 31 ambalo linatakiwa kuwa la mchujo.
"Nimewasili. Asanteni kwa mapokezi mazuri ndugu zangu Wakenya, kama bado hujapata tiketi yako hujachelewa," Alisema..
Alipokelewa na Daniel Ndambuki wa Churchill Show maarufu kama Mwalimu Churchill.
Pia alizawadiwa shada la maua wakati wa kuwasili kwake.
Christina Shusho anatarajia kufanya kolabo na wasanii wengine kama Solomon Mkubwa na Mercy Masika wakati wa tamasha hilo.
Shusho mnamo Novemba aliwahakikishia mashabiki wake kuwa atatumbuiza nchini Kenya.
Kupitia akaunti yake ya X, alisema ameamua kuwa na tamasha kwa ajili ya mashabiki wake wa Kenya kutokana na mahitaji kuongezeka.
Alisema zaidi kwamba timu yake ilikuwa ikiratibu na Mwalimu Churchill kwa ajili ya kuandaa tamasha hilo.
"Kwa sababu ya kuongezeka kwa mahitaji ya tamasha nchini Kenya, timu yangu na mimi tunafanya kazi na Mwalimu Churchill kuwa na tamasha mnamo Desemba 31, 2023.. (Kingereza Kimeisha)," alisema.
Aidha msanii huyo alisema kwamba anafuraha kuwa Nchini, na kuwaalika mashabiki wake kwenye tamasha yake.
"Bwana Yesu Asifiwe Wapendwa.Ninayo Furaha kuwa Nchini Kenya na kwa upendo mkubwa mlionionesha.Nichukue nafasi hii kukualika wewe Rafiki Yangu Garden City tarehe 31.12.2023 crossover.Tutaimba na Kuabudu, watu wataokoka, Mje tumtukuze Mungu.My sister @mercymasikamuguro will be there.@zabronsingers watakuwepo @ngaruiyajunior @solomonmkubwa na pia Born to Worship Team watakuwa nasi.Usikose.Kama uko mbali basi waweza kupata link www.shusho.live."
0 Comments