MUSIC : Dizasta Vina - A father figure (Official Album Intro) Listen/Download

 

Tanzania singers and recording artists better known by his stage names as dizasta vina has released brand new song audio titled a Father Figure enjoy the sound below here



Lyrics
Natazamwa kama mgongo 
Wa kuegewa kama chombo
Nikitegemewa na watoto 
Lakini kwa ndani mi' ni mtoto pia

Mtoto wa katikati
Njiapanda kati ya 
Ukweli na uongo 
Ukubwa na udogo ama
Upofu na uchongo
Ama pumbazo na mwongozo

Katikati ya uhalisia 
Na mategemeo 
Karibu na jitihada 
Mbali na egemeo
Sina hesabu ya mafanikio
Kila kitu ni jukumu na uwepo wangu 
Ndio hukumu yangu ya leo

Sina cha thamani nilichorithi
Ila nilichonacho ni kumbukumbu ya simulizi
Na picha nilizokuwa nazo 
Nilizopewa na wavuja jasho 
Wasakatonge wa mwanzo kwahiyo 
Nigawie masikio  yako 

Macho yalinipa tishio lenye manufaa kwangu
Maana nilishuhudia kufanikiwa na
Kushindwa kwa mashujaa wangu 
Lakini shuhuda zilinifunza

Zilinifunza kuhusu Mashujaa 
Wa karibu na mbali
Wenye nasibu za ghali 
Au watabibu wa kuponya hali 
Na nguvu ya kufukuza shali
Za wadhalimu na waharibifu
Wenye visu vikali 

Mashujaa walisisimua sana
Lakini wapo kadhaa waliokufa 
Na hawakuacha alama
Nilifunzwa kuhusu hawa 

Hawa mashujaa walipanda maua 
Wakilea vyema yakachipua
Na wengine usingizi ulipowachukua
Wadudu wala mizizi wakafukua

Machache yaliyofanikiwa kukua
Ndege waliyachukua
Na mengine hayakuwa mahala pema 
Kwahiyo yalichomwa na jua na kuungua

Oooh hujui walimwengu walisema nini 
Kuhusu hawa shujaa wangu walioshindwa
Walisema Kaharibuu
Kwakuwa shujaa kwa walimwengu
Ni yule anayeweza wakati akifanya
Lakini sio anayeshindwa wakati akijaribu

Kwa walimwengu shujaa 
Ni yule mwenye nguvu 
Asiyetoa chozi wakati wa uchungu 
Asiyekosa au anayeonekana mtukufu 
Kwa walimwengu ushujaa ni  
Kuweza na sio kuthubutu

Kwahiyo wakati sherehe za mashujaa
wao zikipikwa kuchochea
Hadithi za mashujaa wangu
Zilizikwa na kupotea

Kwakuwa mashujaa wangu 
Hawakuvaa suti zenye nakshi na kuita
Hawakuwa na viatu vya kung'ara hivyo 
Hawakupendeza kwenye jarida

Ni kama walipima ushupavu wa mashujaa 
Kwa kuangalia afya za maua
Bila kujua afya za maua sio ubora
Wa anayeyajua pekee
Lakini kuna jua na mvua  na ni 
Ubashiri wa kujua lini vinakuja 
Uhakika ni kesho, kesho yenye giza 
Na hakuna anayeitambua

Shujaa wangu alileta mlo mmoja 
Kuhakikisha siku haipiti, na aliweka
Tofali Moja wakati wa kujenga msingi
Alifagia barabara alipambana na 
Uraibu kama kamali, ulevi na madawa 
Ila hadithi yake haikuvutia gazeti
Sio sawa

Ni vile nimeanza kuwa kama shujaa
Wangu nimegundua kuwa sijamaliza kujua
Ni kama nimeanza kulea wakati sikumaliza kukua

Natamani kuwa shujaa mzuri
Lakini nipo hapa kujifunza 
Na pa kuanzia sipajui

Sipajui maana maelekezo ni mengi saa hii
Mara jikaze wewe, baba halii
Mara utapoteza nafasi, watu hawatanii
Mara kwanini usifanye kama nanihii
Ona watoto wake wamenanihii

Bahari ya elimu ni pana kuushinda upeo
Kulia matarajio, kushoto mategemeo
Bado najifunza sipo mbali
Ila sijui lini nitakuwa tayari

Inaniwia kuweka kipimo 
cha kujua kipimo kiundani
Kupima usahihi wa wito 
Ninaposema hadharani
Unawaandaaje watoto kwenda mitaani 
Kwa sababu kuliko kuwa mkata maua vitani
Ni bora kuwa mwanajeshi kwenye bustani

Nini maana ya kuwa baba
Ikiwa bado najifunza 
Kutosherehekewa nikishinda 
Ila kusakamwa nikianguka
Hata nikipendwa au nikichukiwa 
Ni sawa ila si vyema nikapuuzwa
Labda ninachelewa ila ni vyema
Nimejua kuwa baba hazaliwi
anaundwa

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE