Mtanzania wapili auawa Israel Makamba afunguka

 

DODOMA: WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema amejulishwa na Serikali ya Israel kwamba kijana wa Kitanzania, Joshua Mollel aliyekuwa anasoma nchini Israel ameuawa mara tu baada ya kutekwa na kundi la Hamas mnamo tarehe 7 Oktoba 2023.


Kupitia taarifa ya waziri huyo inaeleza Serikali ilifanya jitihada kubwa ya kumtafuta kijana huyo ambaye ilipoteza naye mawasiliano tangu tarehe 7 Oktoba 2023.


“Nimeongea na Mzee Mollel, baba mzazi wa Joshua, kuhusu ujumbe huo wa Serikali ya Israel. Tunaendelea na mpango wa awali wa kuwapeleka Mzee Mollel na mwanafamilia mwingine pamoja na Afisa wa Serikali nchini Israel.


“Kuungana na Balozi wetu na maafisa waliopo huko, kukutana na kuzungumza na mamlaka za nchi hiyo ili kupata taarifa za ziada.” Imeeleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa.


Kwa ridhaa ya familia, na itakapobidi, tutatoa taarifa za ziada katika siku zijazo.


Tangu kuanza kwa mapigano ya mwaka huu kuanzia Oktoba 07, watanzania wawili wameripotiwa kufa, mwingine akiwa ni Clemence Mtenga ambaye alikuwa miongoni mwa wanafunzi 260 waliokwenda nchini Israel kushiriki mafunzo ya vitindo ya ukulima wa kileo.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE