WATU 16 wameuawa katika shambulizi Kaskazini mwa Nigeria baada ya kutokea mapigano kati ya wafugaji na wakulima, taarifa ya mtandao wa Reuters imeeleza.
Shambulio hilo lilitokea usiku wa Jumamosi katika kijiji cha Mushu jimbo la Plateau, Kapteni wa jeshi Oya James aliuambia mtandao wa AFP.
Eneo hilo liko kwenye mstari wa kugawanya kaskazini mwa Nigeria wenye Waislam wengi na Wakristo wa Kusini na kwa miaka mingi imekuwa ikipambana na mivutano ya kikabila na kidini hata hivyo haijabainika chanzo cha shambulio hilo.
Askari wa usalama walitumwa ili kuzuia mapigano katika eneo hilo, ambapo mauaji ya kupigwa risasi kati ya wafugaji, ambao mara nyingi ni Waislamu, na wakulima, ambao kwa ujumla ni Wakristo, mara nyingi huingia kwenye uvamizi wa vijiji unaofanywa na magenge yenye silaha kali.
Gavana wa jimbo, Caleb Mutfwang alilaani shambulizi la hilo aliloliita “la kinyama la kikatili na lisilofaa” na kuapa kuwafikisha wahusika mbele ya sheria, msemaji wake, Gyang Bere, aliwaambia waandishi wa habari.
“Hatua madhubuti zitachukuliwa na serikali ili kuzuia mashambulio yanayoendelea dhidi ya raia wasio na hatia,” gavana huyo alisema.
0 Comments