Mambo 5 ya kuzingatia unapotafuta mpenzi mitandaoni


 1. Unapoanza kuwa na hisia na mtu, kumbuka kwamba ikiwa hamjawahi kuonana ana kwa ana, hisia hizo sio halali. Kwa kuwa akili yako haina habari na taswira halisi kuhusu mtu huyo, kama ambavyo ungekuwa kama mngeonana ana kwa ana.

2. Usijihusishe tu katika mahusiano ya kimtandao. Ni sawa kuanza kumjua mtu kupitia anachokiandika, lakini hatua hii haipaswi kuendelea kwa muda mrefu. Ili kuweza kumjua mtu vizuri ni vyema ukapanga kukutana naye mda mfupi baadaye.

3. Usijenge uhusiano na mtu anayeishi katika nchi tofauti. Kuwa na uhusiano na mtu ambaye yupo nchi nyingine na hakuna uwezekano wa kuwa pamoja ni kujitesa. Watu ambao hufanya hivi hushiriki katika mapenzi ya kufikiria.

4. Sahau juu ya watu ambao wameoa. Usikubali kuanzisha mahusiano na watu hawa hata wakisema uhusiano uko karibu kuisha. Watu wengi wamejiingiza katika udanganyifu wa aina hii. Ikiwa una uwezo wa kuanzisha uhusiano na watu ambao huna haja ya kusubiri watengane kwanini uhatarishe kwa kusubiri mahusiano mengine yaishe ndipo wewe uingie itakuwaje kama watarekebisha tofauti zao .

5. Kumbuka kwamba huwezi kujua ni mtu wa aina gani unazungumza naye. Mtu yeyote anaweza kuwa mkarimu, anayejali na makini kupitia skrini. Lakini nyuma ya skrini hiyo inaweza kumficha mtu aliye na matatizo mengi ambayo kimsingi unaweza kushindwa kuendana naye.

Credit: Jamii Forums

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE