DAR: Serikali imebomoa makazi ya eneo la Kijijini lililopo Kata ya Kawe, Mtaa wa Mbezi Beach B, Wilayani Kinondoni ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mkuu wa Wilaya, Saad Mtambule aliyetoa siku 14 (hadi Novemba 17, 2023) akiwataka wakazi wahame kwa hiari kwa kuwa wapo katika Hifadhi ya Barabara
Eneo hilo liliripotiwa kukithiri kwa biashara haramu ikiwemo uuzaji wa Dawa za Kulevya (unga), Bangi, pombe za kienyeji na biashara ya ngono
Awali, Wakazi hao waligoma kuondoka huku ikidaiwa baadhi yao waliagiza Mganga wa Kienyeji kutoka Mtwara awafanyie zindiko wasiweze kuondoka eneo hilo
0 Comments