Mafuriko mengine yaripotiwa Babati, nyumba 13 zikisombwa na maji

 Wilaya Ya Babati Mkoani Manyara imekumbwa Na Mafuriko Hususan Katika Kata Za Dareda, Ari Na Dabil kusababisha athari kwa wananchi, miundombinu ya barabara huku Kaya 13 Zikipoteza Makazi.


Waathirika wa mafuriko hayo wanasema yametokea usiku wa kuamkia Desemba 9, 2023 baada ya mvua kubwa kunyesha ambayo ilisababisha mafuriko yaliyowaacha bila makazi, huku wakiiomba serikali kuwasaidia. Katibu tawala wa wilaya ya Babati Khalfan Matipula ametembelea eneo hilo akiwa na wadau wa misaada mbalimbali na kubainisha kuwa tayari kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya imefanya tathmini ya kaya zilizoathiriwa na mafuriko hayo.


Mafuriko hayo yanatokea ikiw ani siku chache kupita tangu kutokea mafuriko ya maporoko ya udongo yaliyoambatana na mvua kubwa na kusasabisha vifo vya watu Zaidi ya 80, na majeruhi kadhaa katika wilaya ya Hanang mkoani Manyara.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE