Maambukizi ya VVU Mara yongezeka

 Imeelezwa kuwa Kiwango cha maambukizi ya Ukimwi mkoani Mara kimeongezeka kutoka asilimia 3.6 miaka mitano iliyopita hadi kufika asilimia 5 mwaka jana.



Takwimu hizo zimetolewa leo, Desemba 12, 2023 na Mratibu wa Upimaji Ukimwi na Tohara Kinga Mkoa wa Mara, Felix Mtaki kwenye mafunzo ya waandishi wa habari yaliyoenda sambamba na utambulisho wa mradi wa Afya Thabiti.


Amesema uwepo wa mtandao wa wanaofanya biashara ya ngono ni sababu nyingine iliyochangia ongezeko hilo na jamii ina jukumu kubwa la kufanya kwenye mapambano hayo badala ya kuiachia Serikali na wadau.


Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi Mkoa wa Mara, Dk Omari Gamuya amesema ipo mikakati kadhaa inayotekelezwa mkoani humo ili kuhakikisha kasi ya maambukizi mapya inapungua.


Amesema huduma bora kwa wagonjwa wa Ukimwi ni moja ya mikakati hiyo ambapo amesema Serikali hivi sasa imeboresha huduma hasa za tiba kwa wagonjwa hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza maambukizi mapya.


Amesema mradi wa Afya Thabiti unaotarajiwa kutekelezwa kwa muda wa miaka mitano mkoani Mara chini ya Amref ni moja ya mikakati ya kupambana na ugonjwa huo na kwamba mradi huo utahusisha masuala ya kinga na huduma za tiba.


0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE