JITIHADA Ni Msingi wa Mafanikio

 Kazuo Inamori, nguli wa Kijapani anakufundisha mambo 11 ya kuzingatia ili jitihada zako zizae matunda.




1. Kazi ni utu. 

Jitahidi sana kufanya kazi.

Popote pale ulipo. Anzia hapo.

Kazi itakupa thamani maishani.

Sio lazima uajiriwe. Fanya kazi.

Mengine yatajipa mbele ya safari. 


2. Usikubali kukwamishwa na vikwazo.

Maisha ni vita. Unapokubali kukwama unakuwa umekubali maisha yamekushinda.

Usikubali kutoka relini.

KOMAA.


3. Daima tafuta kuanza enzi mpya ili kuwa na kitu cha kukimbiza maishani.

Ukiona jambo haliendi vile inafaa, jitafute na uanze enzi mpya.


4. Penda kazi yako.

Fanya kazi inayokupa satisfaction moyoni.

Usifanye tu kazi alimradi maisha yaende.

Kwa kuanza unaweza kuanza na kazi ya ku-survive.

Ukijipata hakikisha unafanya unachopenda. Au basi penda unachofanya. 


5. Makinikia jambo moja.

Ni jambo jema kujua vitu vingi.

Unaweza kujua mambo mengi sana.

Jitahidi kuwa mtaalam wa jambo moja kwa undani sana. 

Yaani kuwe na eneo, watu hawawezi kutoboa bila wewe.


6. Fungua njia yako mwenyewe.

Mara nyingi huwa tunahitaji msaada wa watu waliotutangulia.

Mara nyingi huwa tunatafuta kazi za kuanzia.

Ukumbuke malengo ni kufungua vyetu na kuwagusa wengi zaidi.


7. Akili nzuri - mwili mzuri.

Kula vyema jenga mwili wako.

Unakuwa na ustawi kulingana na kile unakula na kuweka maishani mwako.

Kula vyema, jenga afya yako na ustawi wa akili.


8. Daima jihoji kwenye maisha yako.

Usikubali kuishi bila dira.

Weka malengo yako.

Kumbuka kujitafakari na kujihoji mwenyewe.

Hii itakupa majibu ya maswali mengi magumu.


9. Soma vitabu vizuri upanue upeo wako.

Kusoma vitabu ni mentorship ya kiaina.

Unaingia maishani mwa mtu na kujifunza kupitia maisha yake.

Usipoteze nafasi hii. Soma vitabu,

Iba siri za ushindi. 


10. Daima ishi kwa kuwatia wengine moyo.

Usiwe mchoyo. Usitake kutoka mwenyewe.

Kama una vijana wako chini yako.

Hakikisha unakuwa kiranja wa kweli.

Wafundishe na watie moyo wa kupambana.


11. Jenga uaminifu na uishi daima.

Uaminifu ni mtaji. Jiaminishe.

Tunazijua stori nyingi za watu waliofanikiwa kwa kuonesha uaminifu tu.

Kosa vyote kwa jamii, lakini usionekane usie mwaminifu.


Usisahau kushare Wengi Wajifunze!


0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE