Vipimo
Viazi (mbatata) - 2lb
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - Kijiko 1 cha chakula
Chumvi - Kijiko 1 cha chakula
Pilipili ya kusaga - kutegemea na unavyoipenda
Ndimu - 1
Mafuta ya kupikia
Unga wa dengu au Ngano - Kiasi.
Namna ya kutayarisha na kupika
Chemsha viazi mpaka viwive, kisha vitoe maganda na uviweka ndani ya bakuli.
Vipondeponde kwa mkono mpaka viwe laini.
Saga thomu na tangawizi kisha changanya na viazi.
Weka chumvi, ndimu na pilipili ya unga, changanya vizuri kisha uonje, unaweza kuongeza viungo hivi kwa kadri ya mapenzi yako.
Tengeneza madonge ya duara uyapange katika tray.
Vuruga unga wa dengu au ngano kwa maji uwe mwepesi kidogo.
Weka mafuta ya kupikia ndani ya karai na uliweke kwenye moto.
Chovya madonge kwenye unga na uyatose kwenye mafuta ya moto. (Uchomaji wake ni kama kuchoma bajia)
Wacha kachori zibadilike rangi kuwa ya njano na uzitoe kwenye mafuta.
Weka Kachori kwenye sahani zipoe tayari kwa kuliwa.
Kidokezo.
Ni nzuri sana kuliwa kwa chatne, au kwa kuchanganywa kwenye mix ya bajia na mbatata za rojo.
0 Comments