Vipimo
Nyama ya kusaga - 2 LB (Ratili)
Mayai - 6
Vitunguu - 4
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 1 Kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai
Nyanya iliyokatwa katwa - 4
Kotmiri - ½ Kikombe
Pilipili Manga - ¼Kijiko cha chai
Bizari ya curry - ½ Kijiko cha chai
Nyanya ya kopo - 3 Vijiko vya supu
Garam masala - 1 Kijiko cha supu
Mafuta ya kukaangia - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chemsha mayai, yakiiva ambua maganda na uweke kando.
Katika sufuria weka mafuta yapate moto, Kaanga vitunguu hadi vigeuke na kuwa rangi ya hudhurungi.
Halafu tia thomu na tangawizi kanga kidogo tu, kisha tia bizari zote na pilipili uendelee kukaanga.
Kisha weka nyama na uiache motoni huku unakoroga hadi iwe si nyekundu tena.
Tia nyanya na chumvi ziache zilainike halafu tia nyanya ya kopo.
Ongeza maji kiasi unavyopenda mchuzi wako kuwa mzito au mwepesi.
Kisha weka yale mayai ya kuchemsha na iache itokote kidogo kwa moto mdogo.
Mwishoe mwagia kotmiri, changanya na umimine katika bakuli na itakuwa tayari kwa kuliwa na wali au mkate upendayo.
0 Comments