Ghasia zaikumba Guinea baada ya bohari ya mafuta kulipuka na kuuwa watu wasiopungua 23


 Askari usalama wa Guinea jana Alhamisi walikabiliana na vijana walioandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Conakry wakitaka kurejeshwa uuzaji mafuta ya petroli katika vituo mbalimbali katika mji huo mkuu ambavyo vilisitisha huduma hiyo baada ya mlipuko mkubwa katika bohari kuu ya mafuta nchini humo.


Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa mapigano ya hapa na pale yalizuka jana mchana kati ya makundi ya vijana waliokuwa wakirusha mawe na vikosi vya usalama vilivyolipiza kisasi kwa kuwarushia mabomu ya machozi huko Conakry mji mkuu wa Guinea. Mamia ya waandamanaji vijana waliweka vizuizi barabarani katika maeneo kadhaa kuelekea katikati mwa mji mkuu huku wakimwaga taka na kuchoma matairi. 



Vijana wa Conakry wapambana na polisi wakitaka kurejeshwa huduma za mafuta ya petroli 

Aghalabu ya vijana hao walioandamana hujipatia riziki kwa kujishughulisha na uendeshaji pikipiki na wametoa wito wa kufunguliwa vituo vituo vya mafuta huko Conakry. Serikali ya Guinea kwa upande wake jana ilisema kuwa mlipuko mkubwa uliombatana na moto katika bohari kuu ya mafuta ya serikali Jumatatu hii katika wilaya ya Kaloum inayopatikana huko Conakry karibu na bandari umeuwa watu 23 na kujeruhi 241. 


Serikali ya Guinea imesema kuwa inaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini kama kuna waathirika zaidi wamesalia. Kanali Mamady Doumbouya Mkuu wa utawala wa kijeshi wa Guinea Conakry ambaye alitwaa madaraka kupitia mapinduzi ya mwaka juzi ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia jana. 

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE