Sickle cell anemia au Seli mundu.
Ni aina ya ugonjwa wa kurithi ambao huathiri seli nyekundu za damu na vibeba oxygen kwenye damu vinavoitwa haemoglobin.
Ugonjwa huu hutokea pale mtu anaporithi gene beta-globin zilizoathirika kutoka kwa mzazi wake. Gene hizi zinaathiri moja kwa moja ufanyaji kazi wa seli nyekundu za damu.
Kutokana na kwamba ugonjwa huu ni wa kurithi hivo unaweza kuambukizwa kupitia kizazi kimoja hadi kingine.
Kwanza ni muhimu kufahamu haemoglobini ni nini...??
》Haemoglobin ni kiambata cha protein kilichopo kwenye seli nyekundu za damu. Kazi yake ni kubeba hewa safi ya oxygen na kuisafirisha sehemu mbalimbali za mwili kupitia kwenye damu.
》Kwa mgonjwa wa siko seli, seli zake nyekundu zinakuwa na umbo la mundu ama mwezi nusu. Kitu ambacho siyo cha kawaida kwani seli nzima huwa na umbo la mduara.
》Seli hizi za damu zenye umbo la mundu zinapata ugumu kusafiri kwenye mishipa ya damu kutokana na umbo lake.
》Na ndipo hupelekea seli hizi kuvunjika na kukwama njiani kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kusafiri na hivo hewa safi ya oxygeni haifiki sehemu mbalimbali za mwili.
NB: Twende Pamoja nikupe shule itakusaidia na kizazi chako, Hakikisha umeshea na wengine wafaidike.
Kuna aina karibu tatu za siko seli, ikiwemo hii ya siko seli anemia.
》Ifahamike kwamba uwepo wa seli mundu baadhi zilizoathirika kwenye damu basi siyo kigezo kwamba seli zote nyekundu za damu zitakuwa na umbo la selimundu.
》Lakini kadiri muda unavosogea ndivo seli mundu nyingi zaidi zitakavoongezeka.
》Seli nzima za damu huchukua siku 120 kufa lakini seli mundu ni siku 20 tu. Jambo hili husababisha upungufu mkubwa wa damu kwa mgonjwa na pia kukosa hewa safi kwenye mwili.
Kwanini watu huugua sickle cell anemia..?? 》Kama tulivosoma hapo juu ugonjwa wa siko seli ni wa kurithi. Hivyo hausababishwa na mazingira au mtindo wa maisha. 》Kwa mtoto kupata siko seli lazima arithi baadhi ya gene zilizoathirika. 》Hivyo basi ikitokea mzazi mmoja ame athirika basi watoto wake watarithi gene hizo, Lakini ugonjwa na dalili hazito onenaka mpaka pale, Mtoto akipata mzazi mwezi ambae nayeye alibeba gene zilizo athirika. 》Basi mtoto atakayezaliwa atakuwa na siko seli anemia na dalili zake zitakuwa zinajionesha. NB: Na ndiyo maana tunashauri kufanya vipimo kabla ya kuzaa, Asilimia kubwa ya wanao pitia changamoto hii, Hawana uelewa wa ku check afya.
Dalili na viashiria kwamba tayari unayo siko seli anemia.
》Kama tulivosoma hapo juu, ugonjwa huu wa siko seli anemia unasababisha kukwama kwa damu kwenye mishipa ya damu.
》Hali hii husababisha maumivu na dalili zingine mbaya ambazo zinaathiri shughuli za kawaida za viungo mbalimbali vya mwili kama figo, ubongo, mifupa, bandama na vingine.
》Kila mgonjwa mwenye sikoseli anemia basi hupata upungufu wa damu mara kwa mara. Wagonjwa wengi wa siko seli hupata dalili zingine kama;
1. Kuvimba mwili na kujaa maji.
2. Kupata homa kali mara kwa mara.
3. Uchovu mkali na mwili kuchoka sana.
4. Kupata shida ya kupumua na maumivu ya kifua na hivo mgonjwa kupoteza uchangamfu.
5. Maumivu ya mifupa na joints: kupungukiwa kwa uroto (bone marrow) kwenye mikono na miguu na hivo kuleta maumivu makali.
6. Kuathirika kwa usafirishaji wa virutubisho na hewa kwenye damu husababisha Ngozi kupata malengelenge.
7. Ngozi kuwa ya njano kutokana na kuongezeka kwa nyongo kupita kiasi kwenye bandama.
8. Kushindwa kushiriki ngono ipasavyo, mfano wanaume hupata maumivu uume unaposimama.
9. Wagonjwa wa siko seli wapo kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi kama nimonia(pneumonia) kutokana na bandama kutofanya kazi vizuri
10. Pia wagonjwa wa siko seli wana hatari zaidi ya moyo kupanuka kutokana na kuongezeka kwa presha kusukuma seli za damu zilizokwama kwenye mishipa ya damu.
NB: Ni kushuka wewe ulisoma makala hii mpaka mwisho, Nikusisitize jambo moja afya yako ndio msingi wako, Usipange kukosa next lesson dhidi ya matibabu ya siko seli anemia.
endelea kuwa nasi mpaka tukutane tena
0 Comments