Uzazi wa mpango ni matumizi ya vidonge, Sindano, Vipandikizi, kitanzi, Condom na Callender. Njia hizo zinasaidia kuepuka mimba zisizotarajiwa.
1. Kitanzi: Husetiwa katika tumbo la uzazi, hufanya kazi kwa kuzuia yai lisirutubishwe na mbegu za kiume kwa kutengeneza utandu mzito,
Kitanzi hudumu kwa miaka 12 baada ya kuwekewa. Njia hii haina Vichocheo vya aina yeyote.
2. Vipandikizi: Vipo vya aina mbili cha miaka 3 na miaka 5, Njia hii inayo vichocheo vinavyo fanya kazi ya kuzuia kupevuka kwa mayai.
3. Sindano: Njia hiii hufanya kazi kwa kutegemea vichocheo, Ukitumia njia hii uta dugwa sindano kila baada ya miezi mitatu.
4. Vidonge vya majira: Vipo vya aina 2 COC Na POP, Aina moja inayo mchanganyo wa vichocheo viwili, Aina nyingine inayo aina moja tu ya vichocheo mwilini.
Unatakiwa kumeza vidonge kilasiku bila kuruka hata siku moja, hata kama mwenza wako hayupo siku hiyo.
5. Condom: zipo zaaina 2 zakike na zakiume faida moja wapo ya matumizi ya Condom ni kuzuia mimba na magonjwa ya zinaa.
JE..? Una uelewa gani kuhusu njia hizo za uzazi wa mpango...?
JE..? Una swali lolote kuhusu matumizi ya uzazi wa mpango...?
JE..? Wewe na mwenza wako mnatumia njia gani ya uzazi wa mpango..?
0 Comments