Clamcris afunguka alivyowachenga Bodi ya Filamu akanaswa na polisi

 Mwigizaji wa vichekesho nchini, Ridhiwani Juma @clamcris_ amefunguka alivyokamatwa na maafisa wa Bodi ya Filamu Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi baada ya kukiuka maagizo aliyopewa na taasisi hiyo.



Bodi ya filamu nchini Tanzania iliwakama na kuwafungulia kesi polisi Ridhiwani Juma na mwenzake Stering Makoti @kicheche_ kwa makosa ya kurusha maudhui yanayoenda kinyume na maadili.


Inadaiwa waigizaji hao walitakiwa kuwa wanapeleka kazi zao bodi ya filamu zihakikiwe kabla ya kutoka lakini wamekuwa wakikaidi kanuni hizo.


“Walikamkamata Kicheche kwanza kama wiki mbili nyuma baadaye akatoka, nikawa natafautwa mimi sasa na hapo nilikuwa mkoani niki-shoot ‘Snake Boy’, kwa hiyo wakanifuata wakanikamata na kunieleza kwa nini wamenikamata.



“Tukio lilivyo, tuliwahi kuitwa Bodi ya Filamu baada ya kutengeneza clip ambayo haikuwa na maudhui mazuri, baada ya kuitwa tulipewa maelekezo kuwa tuwe tunapeleka clip zetu zikaguliwe kabla ya kurushwa lakini hatukufanya hivyo.


“Kwa hiyo hata kututafuta walikuwa wanatutafuta kimya kimya, sababu wangeweza hata kutangaza kama tunawatafuta watu flani. Walikuwa wananipigia simu lakini mimi sipokei namba ngeni, ikawa kipengere kunipata.


“Wakaangalia namna yao wanayoweza kunipata, wakanipata wakanikamata na tukaenda kituoni. Wao ni walezi, tuliyazungumza yakaisha,” amesema Ridhiwani.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE