Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema limemfutia adhabu ya kutofanya shughuli za Sanaa Mwanamuziki Hamad Ally maarufu Madee mara baada ya Msanii huyo kulipa faini na kurekebisha wimbo wake kama alivyotakiwa katika tamko la kupewa adhabu.
Ikumbukwe, December 14, 2023 Baraza la Sanaa la Taifa kupitia Sheria Na. 23 ya Mwaka 1984 a Marekebisho yake ya Mwaka 2019 Kifungu cha 4(p) ilitoa adhabu kwa Mwanamuziki huyo mara baada ya kuchapisha wimbo (Unaoitwa Nakojoa Pazuri) wenye maudhui yanayokiuka kanuni za BASATA za mwaka 2018 na Mwongozo wa uzingatia maadili katika kazi za Sanaa wa mwaka 2023.
Aidha, Msanii huyo ameruhusiwa kuutumia wimbo wake uliorekebishwa katika shughuli zake za Sanaa ikiwemo kuchapishwa katika mitadao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali (digital platforms).
“Baraza halitavumilia ukiukwaji wowote wa Maadili katika shughuli za Sanaa hivyo linawataka Wasanii wote kufanya kazi zao kwa mujibu wa Mwongozo wa uzingatia maadili katika kazi za Sanaa wa mwaka 2023 unaopatikana katika tovuti ya BASATA pamoja na nakala ngumu ofisi ya BASATA”
0 Comments