Mamia ya wanaume katika mtaa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam nchini Tanzania wamejitokeza kwa wingi kuandamana kama ishara ya kulaani na kupinga vikali hatua ya serikali kufunga madanguro ya warembo wanaochuuza ngono.
Kwa mujibu wanaume hao, serikali ilifanya vibaya kuwafungia sehemu zao za starehe kwani hawashrutishwi kwenda kule wana hawaendi pale kuibiwa.
Baadhi walisema kwamba madanguro hayo ndiyo sehemu zao za kukata kiu na mwisho wa simu yakiendelea kufungwa watalaumiwa kubaka.
“Sasa itakuwa vipi, mwisho wa siku unaweza ukashangaa tukabaka, au sio bwana. Kwa sababu sisi tunatafuta hela tunaenda pale tunatoa hela zetu. Sio kwamab tunawakamata au vipi, ni hela yetu tunatoa na tunaridhika tu,” mmoja alisema huku akikanusha takwa la kuoa ili uepuka uzinzi.
“Watu tunashauriwa tuoe ndio, naweza kuwa nyumbani nina mke lakini kwa sababu ya sisi wanaume tulivyo, mke wangu nyumbani naweza nikamuacha nakuja napiga kimoja naenda ofisini,” aliongeza.
“Tunalalamika kwa sisi walala nje au tuseme tusio kuwa na wanawake. Hawa ni kipozeo chetu sisi ili tusipate vishawishi vya nje kumbaka mwanamke au nani. Ukitoa elfu 2 au 3 yako unatoa ugumu wako maisha yanaendelea,” mlalamikaji mwingine alisema
Hatua hii inafuatia siku chache tu baada ya RC wa mkoa wa Pwani ya Tanzania, Albert Chalamila kufanya kikao na wakuu wa wilaya zote za mkoa huo na kuafikiana kuleta stara katika jiji hilo.
Chalamila alisema kwamba maeneo yote ya masaji na wanawake kutingisha makalio yalikuwa ni marufuku kuanzia wiki hii kwenda mbele, akisema kuwa ni njia moja ya kurudisha maadili mema katika jamii ambayo imepotoka.
0 Comments