Ukifuata haya mambo 6 kwa miezi 6 utakuwa mbali sana.


 Huhitaji kujisikia kufanya jambo.

Ili kufanikiwa inabidi uwe umevuka hiki kipimo. Kila siku utaenda na kujenga ndoto yako bila kujali uko kwenye mood au la. Kila siku utahakikisha umesogeza kete ya mafanakio kulingana na plan yako. Sio la kujiskia au kutojisikia. Punguza muda wa kusoma na wekeza kwenye application. Kujifunza kunakuwa na tija kama unatumia maarifa. Sio kila siku ni kusoma kozi, vitabu na kuhudhuria conferences - TUmia maarifa yako. Growth inakuja kwenye kuapply maarifa kwenye hali halisi ya maisha. Usitumie muda mwingi kutafakari. ANZA. Kuna kipindi unakuwa unataka kufanya kitu, umefanya utafiti na kila kitu kiko sawa lakini huanzi. Kunakuwa na kasauti ka ndani kanakwambia, huwezi. Kasauti ka ndani kanakwambia wewe mbona utafeli tu, acha upuuzi. Ni wakati wa kujitambua na kwendea ndoto zako. Acha kusitasita, mwisho wa siku maisha ni gemu tu, kuna kupata na kukosa. Go for it. Acha kulalamika na kulaumu. Kila unapofungua mdomo wako kulaumu unajiaminisha kuwa huwezi. Kila unafungua mdomo wako kulalamika unajiaminisha kuwa hutoshi. Ukilalamika unakubali kuwa mhanga na kuwa huna kitu cha kufanya. Jiamini kuwa wewe ndiye. Wewe ndiye mwenye balaa. Kila utakachogusa kitanyooka na kuleta matunda. Jiamini. Control hisia zako. Usioe kwa hisia. Usianzishe biashara kwa hisia. Usigombane na mtu kwa hisia. Tumia akili yako. Tumia muda wako kufikiria na kutafuta ufumbuzi. Wanasema ‘kufikiria ni kazi ngumu ndo maana watu wengi hawapendi kufanya’. Think Big. Show up kila siku. Hii ndio ibada yetu. Moja ya ushindi kwenye maisha yako ni kutowahi kukata tamaa. Unaweza kufeli mara kadhaa na kuacha projects zako. Endelea. Dhambi kubwa ni kukata tamaa. Kutoboa maana yake ni kutokata tamaa. Pambana. Komaa. Iko siku njema inakuja. Kumbuka hakuna asiyependa kitu pesa. Itafute sana. Itakuheshimisha.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE