Matokeo ya mtihani wa KCPE kutolewa kabla ya Krismasi

 Wizara ya Elimu imetangaza mipango ya kutoa matokeo ya mtihani wa darasa la nane (KCPE) mapema ili kuwapa wazazi muda wa kujiandaa.



Kulingana na Wizara mtihani huo utatolewa katika muda wa wiki chache ili kuruhusu wanafunzi kuchagua shule kabla ya Krismasi.


Kulingana na katibu wa kudumu wa Elimu ya Msingi Dkt Belio Kipsang, usahihishaji wa KCPE umeanza huku matokeo yakitarajiwa kutoka baada ya wiki chache.


Akizungumza baada ya kuzuru shule ya upili ya wasichana ya Naivasha, Belio aliwapongeza walimu wakuu kwa kazi waliyofanya wakati wa mitihani ya kitaifa.


"Tunatarajia matokeo yatoke mapema ili upangaji wa wanafunzi katika kidato cha kwanza ufanyike kabla ya Krismasi na wazazi wapate muda wa kutosha wa kujiandaa," alisema.



Wakati uo huo Kipsang alipepezea chini visa vya hivi majuzi vya wizi wa mtihani wa KCSE na kuongeza kuwa ni wasimamizi saba pekee wa vituo waliosimamishwa kazi.


Alisema kumekuwa na visa vichache mno vya wizi mitihani mwaka huu kutokana mfumo wa kuchukuwa karatasi za mitihani mara mbili kwa siku pamoja na ushirikiano wa karibu na idara ya usalama.


"Tuligundua kuwa kulikuwa na ufichuzi wa vifaa vya mtihani ulipochukuliwa mara moja na kupelekea hatua ya kuichukuwa mara mbili kwa siku," alisema.



Katibu huyo wa elimu alisema kuwa wasimamizi saba wa vituo ambao walikuwa wamesimamishwa kazi na watachukuliwa hatua za kinidhamu mara tu mitihani itakapokamilika.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE