Mafuriko Yaharibu Mboga Na Nyumba Za Wenyeji Wa Kijiji Cha Wahambla

Wenyeji wa kijiji hicho sasa wana hofu huenda wakakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.



Wamekuwa pia wakiuza mboga ili kujipatia hela kiasi za matumizi.

Mbali na sukumawiki, wakulima hao wamekuwa pia wakipanda nyanya na vitunguu.


Chifu wa lokesheni ya Kanyada Mashariki John Ndiga amesema pia mvua iliyopitiliza imeharibu nyumba na kuathiri familia 35 katika kijiji hicho. Wengi wao walihamia katika eneo la mwinuko la barabara ya Kendu Bay-Homa Bay usiku wa kuamkia leo Jumamosi.


Hata vyombo vya nyumbani vimefagiliwa na maji ya mafuriko hadi katika Ziwa Victoria.


“Nyumba nyingi zilizoharibika ni za udongo. Kuta ziliporomoka na kufagiliwa na maji,” Bw Ndiga amesema.


Anatarajiwa kuikabidhi ripoti kwa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini (KRC) na idara ya kukabili majanga ya Kaunti ya Homa Bay.


Familia nyingine zimepoteza kuku na ndege wengine wa nyumbani.


Mzazi, Bw Moses Akello amesema vitabu vya watoto wake vimeloa maji.


“Ingawa wanaenda kwa madarasa mengine mwaka ujao, vitabu vilivyoharibiwa na maji vingewafaa sana,” amesema Bw Akello.


Mkulima wa nyanya, Bw Kelly Ochieng, amesema alikuwa ametumia zaidi ya Sh35,000 kustawisha kilimo cha zao hilo. Alikuwa akitarajia kuuza nyanya sokoni na kuingiza Sh200,000 lakini sasa mimea yake imeharibika kabla ya msimu wa kuvuna.


0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE