Undani bei za kuongezea makalio Mloganzila

 Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kuanzia October 27,2023 kwa mara ya kwanza nchini itafanya huduma za kibingwa bobezi za upasuaji wa kupunguza uzito na upasuaji rekebishi ambao utahusisha kupunguza mafuta na kurekebisha sehemu ya mwili mfano kupunguza au kuongeza ukubwa wa matiti na makalio, kupunguza tumbo au nyama kwenye mikono na sehemu nyingine za mwili ambapo imetaja bei ya kurekebisha shepu kuwa itaanzia Tsh. milioni 12 hadi milioni 18 ambayo ni nafuu ukilinganisha na nje ya Nchi ambako inafikia hadi Tsh. milioni 70.



Mkuu wa Idara ya Upasuaji Dkt. Eric Muhumba na Dkt. Edward wamesema upasuaji huo utafanywa na Wataalamu wa MNH-Mloganzila kwa kushirikiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa kupunguza uzito na Upasuaji Rekebishi kutoka India, Dkt. Mohit Bhandari pamoja na MedINCREDI.


“Njia tunayotumia kuongeza shepu ni kwa kuondoa mafuta kwenye tumbo na kuweka kwenye makalio yakiwekwa kule anakuwa na shepu nzuri, hips pia tunaongeza kwa kutumia mafuta yaleyale yanayotoka kwenye tumbo, upasuaji huu kwasababu tunahamisha mafuta yake mwenyewe usalama ni mkubwa tofauti na njia nyingine, Muhimbili Hospital haipendi malalamiko ndio maana tunatumia njia salama”


Madaktari hao wamesema mwitikio ni mkubwa sana na wanapokea simu nyingi Watu wakiulizia ingawa bado hakuna aliyelipia kwa ajili ya kuongeza shepu lakini wapo walioonesha nia ya kuongeza na Watu watatu tayari wamelipia kupunguza uzito, gharama zinaanzia Tsh.milioni 12 hadi milioni 18 na mwonekano wa Mtu ndio utaamua bei iweje kwasababu gharama inatokana na muda unaotumika kuhamisha mafuta… video nzima ipo Youtube ya millardayo.


0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE