Mtwara. Hofu imetanda baada ya watu wawili kujeruhiwa na mnyama tembo katika wilaya ya Tandahimba ambaye ni Faraji Rahisi (30) na mwingine ni mtoto wa miaka sita ambaye alikuwa nje ya nyumba yao.
Akizungumzia na Mwananchi kwa njia ya simu Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanal Patrick Sawalla alisema kuwa watu hao waliojeruhiwa wanatoka katika vijiji viwili tofuati.
“Kwa kweli tembo hawajawahi kusikika katika wilaya yetu yaani hata sisi tunashangaa tunasubiri taarifa ya TAWA ili tuweze kujua wametoka wapi”
“Lakini tumetoa rai kwao kwakuwa tumeambiwa na watalaamu kuwa tembo hawataki kelele hivyo tumewasihi wakae majumbani wasipige kelele wala wasiwarushie mawe kwakuwa hawapendi kelele lakini mashairika mbalimbali yapo huko yanatoa elimu ili wananchi wanachukue tahadhari” Kanal Sawalla
Nae Diwani wa Kata ya Chingungwe Juma Hamisi Mdiliko alisema kuwa katika kata yake ni mtu mmoja aliyejuruhiwa ambaye anajulikana kwa jina la Faraji Ismail Rahisi(30) ambapo alikuwa shambani akiendelea na majukumu yake.
“Alikuwa peke yake analima kwakuwa mashamba yetu tumepakana pakana hivyo baada ya kulia ndio majirani wakakimbilia huko na kutoa taarifa kwetu serikali ya kijiji na tukamchukua na kumuwahisha katia kituo cha afya Mahuta ambapo alipata huduma ya kwanza kisha kupelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Tandahimba”
“Sisi hatuko karibu na hifadhi yoyote ndio maana tunashamba kikubwa tunaomba tujue wametokea wapi na elimu itolewe juu ya tembo ili wananchi wajue namna bora ya kujilinda nao kwasasa wamekosa amani”
Nae Mkazi wa Kijiji cha Mdimba Jazal Salum Namchenda alisema kuwa mgonjwa huyo ni ndugu yake na anaendelea vizuri kabla ya tukio alikuwa analima asubuhi saa moja ndio alitokea tembo na kumjeruhi.
kwa mujibu wa mgonjwa hakumuona tembo ila mkewe alikuwa shambani japo mbali lakini alimuona tembo alipojaribu kumwambia mumewe lakini hakumuelewa ndio akajeruhiwa”
“Hatujui tembo katoka wapi hatujawahi kusikia Tembo katika maeneo yale hata sisi tumeshangaa lakini tunahsukuru mgonjwa wetu anaendelea vizuri na leo ameamka salama na amekula chakula bila tatizo
0 Comments