Rais Samia ahani msiba wa Membe

 

Dar es Salaam. Siku 64 tangu kifo cha kachelo mbobezi Bernard Cammilius Membe, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefika nyumbani kwa kiongozi huyo Mikocheni na kwa lengo la kuhani msiba wa mwanasiasa huyo.


Membe ambaye ni waziri wa zamani wa Mambo ya Nje katika Serikali ya awamu ya nne alifariki dunia asubuhi ya Ijumaa Mei 12, 2023 akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kairuki Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu leo, Rais Samia amehani msiba huo leo Ijumaa, Julai 14, 2023 baada ya kufika nyumbani kwa Mama Dorcas Membe ambaye ni mjane wa mwanasiasa huyo mashuhuri, kumfariji na  kusaini kitabu cha maombolezo.


Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Rais Samia amemtembelea na kufanya mazungumzo na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere wakati alipokwenda nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumsalimia na kumjulia hali.


Pia alitumia wasaa huo kumtembelea Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mzee Yusuf Makamba nyumbani kwake Wazo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumjulia hali pamoja na kufanya mazungumzo maalum.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE