Mtafiti mbaroni kushiriki ngono na mwanafunzi

 MKUU wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Julius Mtatiro kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, wamemkamata mkazi wa Mtaa wa Nazareti wilayani humo, David Luya akiwa na msichana wa miaka 12 (jina linahifadhiwa) ndani ya chumba chake. - Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio Mtatiro amesema, Luya alikamatwa majira ya saa 5:30 usiku wa kuamkia jana akituhumiwa kujihusisha kimapenzi kwa muda mrefu na msichana huyo anayesoma shule moja ya sekondari mkoani Dar es Salaam. 


Amesema vyombo vya ulinzi na usalama vilipata taarifa kwamba katika Mtaa wa Nazaret kuna mwanaume mtu mzima amekuwa akijihusisha kimapenzi na kuwadhalilisha wasichana wadogo mara kwa mara. - Mtatiro amesema waliweka mtego na walipofika katika nyumba hiyo walimkuta mtuhumiwa akiwa na mwanafunzi chumbani kwake bila ridhaa ya wazazi. -

 Amesema baada ya kuwakamata wote wawili, kwenye simu ya mtuhumiwa ilikutwa picha ya video ikimuonesha msichana huyo mdogo akiwa chumbani kwa mtuhumiwa akitumikishwa kingono. - Alieleza kuwa baada ya kufikishwa kituo cha Polisi msichana huyo alikiri kuwa amekuwa akitumikishwa kingono na mtuhumiwa kwa muda mrefu pindi wazazi wake wanapoondoka. -

 "Na hata baada ya binti kufanyiwa vipimo vya kitaalamu ilibainika kwamba ameingiliwa kingono na sasa taratibu za kumfikisha mahakamani mtuhumiwa zinaendelea," alisema na kuongeza: - “Huyu mtuhumiwa siyo mwenyeji wa hapa, nadhani mwenyeji wa Mkoa wa Singida ambaye amekuja Tunduru kujihusisha na masuala ya utafiti wa kilimo, lakini tulipewa taarifa kwamba amekuwa na mienendo siyo mizuri kwa muda mrefu na jana ndiyo tumefanikiwa kumkamata.” 

- Mtatiro alisema kukamatwa kwa Luya kumetokana na operesheni kali inayoendelea wilayani humo ya kuwasaka wanaume wanaojihusisha kimapenzi na wasichana wenye umri mdogo hasa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na kusababisha watoto wengi wa kike kuacha shule.


0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE