Katika jamii zetu zimejaa imani tofauti tofauti,Inapo tokea mtoto anakoroma wakati wa kulala utasikia "kamrithi baba au mama yake" pasipo kujua yaweza kuwa chanzo cha ugonjwa fulani
Zifuatazo ni sababu za kukoroma kwa mtoto usiku kama vile
1-Nyama za puani (Adenoids Hypertrophy)
Hizi hupelekea njia ya pua kuwa nyembamba kupitisha hewa ya kutosha na kupelekea mtoto kuwa ankoroma na hata kuwa anashituka wakati wa usiku akiwa amelala , hii inamaana kwaba mtoto anakosa hewa.
2-Unene kupitiliza, mtoto anapokuwa mnene kupitiliza anaweza kuwa anapata shida ya kupumua pia, hii kitaalamu tunaita OBSTRUCTIVE SLEEPING APNEA (OSA) hali hii pia yaweza kupelekea mtoto kuwa anashituka toka usingizini kwa kukosa hewa ya kutosha.
3-Matumizi ya mto kwa mtoto,hii pia inaweza kuwa shida kwani huleta shida kwenye njia ya upumuaji kutokana na mifumo yao ya upumuaji kuwa tofauti na ile ya watu wazima
4-Foregn body (Vitu mfano mbegu ya ubuyu,karanga,maindi,haragwe. n.k ) kwenye njia ya upumuaji mfano pua au koo la hewa -huweza sababisha kukoroma pia
5. Watoto wenye mdomo sungura pia huwa na shida ya kukoroma
Endapo una mtoto anashida kama hii ni vyema kumuona Daktari mapema ili apate tiba kabla ya madhara kuwa makubwa zaidi kujitokeza.
0 Comments