Washawishi wenye utata kwenye mitandao ya kijamii Andrew Tate na kaka yake Tristan wamehamishwa kutoka kizuizini hadi kifungo cha nyumbani kufuatia uamuzi wa hakimu wa Romania.
Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa huko Bucharest unachukua nafasi ya kipindi cha hivi karibuni cha kuwekwa kizuizini, ambacho kilipaswa kumalizika tarehe 29 Aprili.
Washirika wao wawili, Georgiana Naghel na Luana Radu, pia wanaachiliwa. Wote wanne wameamriwa kukaa katika makazi wanayoishi, isipokuwa kama wana kibali cha mahakama cha kuwaruhusu kuondoka.
Msemaji wa ndugu hao wa Tate aliiambia BBC kwamba walikuwa "wamefurahi".
Ndugu hao walifungwa tangu mwezi Disemba wakiwa wanachunguzwa kwa tuhuma za ubakaji, kusafirisha watu kiharamu na kuunda kundi la uhalifu.
Wote wawili wamekanusha kufanya makosa yote. Mawakili wa Bw Tate wamesema kuwa kumweka chini ya ulinzi wa kuzuia ni hfatua ya ukali isiyofaa, wakati chaguzi nyingine za mahakama kama vile kifungo cha nyumbani zinapatikana.
Nyaraka za mahakama zilizovuja, zilizoonekana na BBC, zilieleza ushuhuda kutoka kwa waathiriwa wanaodai kulazimishwa kupata €10,000 (£8,800) kwa mwezi kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii, chini ya madai ya tishio la unyanyasaji wa kimwili.
Nyaraka za mahakama pia zilieleza kuwa madeni yalitumika kama "aina ya shurutisho la kisaikolojia"
0 Comments