Wanachama watatu wa jumuiya ya kidini na kitamaduni nchini Bahrain ambayo inatetea majadiliano ya wazi ya masuala ya Kiislamu wamehukumiwa vifungo jela.
Walifunguliwa mashitaka chini ya sheria ambayo inahalalisha "kejeli" ya maandishi yoyote ya kidini yanayotambulika nchini Bahrain, ambayo ni pamoja na Kurani na Biblia.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema wanaume hao waliteswa kwa kutekeleza haki yao ya uhuru wa kuzungumza
Jumuiya hiyo ilisema kesi hiyo ilichochea vurugu dhidi ya wanachama wake.
Katika mfululizo wa programu zilizochapishwa kwenye YouTube, Jumuiya ya Al-Tajdeed imeibua maswali juu ya nadharia ya sheria ya Kiislamu na maoni yaliyotolewa na maulama wa Kiislamu.
Kundi hilo ni Waislamu wa madhehebu ya Shia, ambao ni idadi kubwa ya wakazi wa Bahrain, ingawa familia inayoongoza ni Waislamu wa Sunni.
Lakini maulamaa mashuhuri wa Shia wamekuwa wakichukia zaidi shirika hilo, wakishutumu kazi yake kuwa ni kufuru na kutaka wanachama wa Al-Tajdeed kutengwa.
0 Comments