Balozi wa Marekani nchini Kenya Meg Whitman anasema Marekani itaendelea kuzilinda haki za wapenzi wa jinsia moja na jamii ya LGBTQI+ kwa ujumla.
Katika ujumbe wake kupitia mtandao wa Twitter Balozi White alisema: “Katika kipindi cha wiki moja iliyopita mimi na timu yangu tulikutana watu wa makundi ya LGBTQI+ na wadau kusaidia haki za kibinadamu za watu LGBTQI+ . Marekani inajivunia kuendeleza juhudi za kuwalinda LGBTQI+ dhidi ya ubaguzi na unyanyasaji na itaendelea kutetea haki za binadamu na usawa,” Balozi Whitman alisema.
Taarifa ya Whitman inakuja wakati rais wa Kenya William Ruto pamoja na viongozi wa kidini nchini humo wakiwa tayari wamepinga hadharani uamuzi wa mahakama ya juu zaidi ulioruhusu usajiri wa mashirika ya LGBTQI+ nchini humo.
Hatahivyo, Balozi Whitman amesema kwamba Marekani haitaingilia msimamo wa Kenya kuhusu suala la wapenzi wa jinsia moja (LGBTQI+) , akisema kuwa kila nchi ina uhuru wa kufanya maamuzi yake kuhusu jinsi ya kushughulia suala la haki za wapenzi wa jinsia moja.
0 Comments