Jeshi la Ujerumani lakabiliwa na ukosefu wa silaha na zana za kijeshi

 Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani imetangaza katika ripoti yake ya siri kwamba, jeshi la nchi hiyo halina uwezo wa kutekeleza majukumu yake ndani ya Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (Nato) kutokana na kukabiliwa na mgogoro wa ukosefu wa silaha, zana za kijeshi na hata sare za askari.



Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kwa kuzingatia hali hiyo jeshi haliwezi kutekeleza misheni zake ndani ya Nato isipokuwa katika eneo dogo tu. Hii ni kwa sababu, kivitendo majukumu yake mkabala wa Nato yameathiriwa na ukwamishaji kiasi kwamba kikosi cha wanamaji cha Ujerumani chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa nacho pia kimeshindwa kutuma hata meli moja katika pwani ya Lebanon.  


Ripoti hiyo ya siri ya Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani imeongeza kuwa, hali ya kimaada na ya utoaji mafunzo kwa jeshi la Ujerumani ni mbaya sana huku zana za kijeshi zinazohitajika kwa ajili ya vita vikubwa zikiwa zimechakaa zikihitaji ukarabati. Hasa ikizingatiwa kuwa sekta inayohusika na silaha na zana muhimu za kijeshi na sare za joto katika Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani kwa ajili ya wanajeshi inakabiliwa na matatizo. 


Hivi karibuni gazeti la Ujerumani la Sud Deutsche Zeitung lilimnukuu Frank Haven, Mkurugenzi  wa Shirika la Masuala ya Ulinzi la Ujerumani - Ufaransa la (KNDS) akisema kuwa hivi sasa jeshi la Ujerumani linakabiliwa na matatizo mengi ya kimaada na  uhaba katika takriban maeneo yote. 


Aidha bi Eva Hogl Kamishna wa masuala ya vikosi vya ulinzi katika bunge la Ujerumani ameeleza kuwa, Berlin inahitaji yuro bilioni 20 ili kuweza kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya vikosi vyake vya ulinzi.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE