Bolton atangaza kuwa tayari kugombea katika uchaguzi ujao wa Rais wa Marekani

John Bolton Mshauri wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Marekani ametangaza kuwa anafikiria kugombea katika uchaguzi ujao wa rais wa nchi hiyo mwaka 2024.


John Bolton amesema kuwa, yupo tayari kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho iwapo wagombea urais wa sasa wa chama cha Republican hawatamkataa Trump. Bolton ameashiria matamshi ya Donald Trump kuhusu katiba ya Marekani na kueleza kuwa, mtu yoyote ambaye anapinga katiba si Mmarekani.  


Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni Trump alitaka kuwekwa kando katiba ya Marekani. Donald Trump amesisitiza katika mtandao wake wa kijamii kwa jina la "The Truth" kuhusu nadharia ya udanganyifu katika uchaguzi wa rais  wa Marekani mwaka 2020 na kutaka kuhitimishwa katiba ya nchi hiyo ili kufuta matokeao ya uchaguzi huo na yeye kurejea madarakani kama rais. 

 

Kuhusiana na hilo, Trump ameandika akihoji: je uko tayari kutupilia mbali matokeo ya uchaguzi wa 2020 na kumtangaza mshindi wa kweli au kuendesha uchaguzi mpya? Udanganyifu mkubwa kama huo ungetoa mwanya na kuruhusu sheria na kanuni zote, na hata yale yaliyomo ndani ya katiba ya Marekani kuhitimishwa na kuwekwa kando.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE