FIFA imeandaa taratibu zikatazotumika viwanjani wakati wa michuano ya Kombe la Dunia 2022, taratibu hizo ni ngumu kuliko miaka ya nyuma.
Mashabiki wametakiwa kuvaa vizuri na kujisitiri haswa maeneo nyeti ya miili yao, pia wameaswa kuwa michoro ya mwilini yani tattoo haitakiwi kuonekana maana ile sio nguo.
Kingine ni kuwa mtu yotote atakayeingia kutizama mechi asiwe kalewa pombe au dawa za kulevya, hili ni kosa kisheria.
Chupa, vikombe, makopo au vitu vyovyote vinavyoweza kurushwa na kuumiza mtu haviruhusiwi viwanjani, pia vyakula vya aina zote haviruhusiwi labda tu awe amebebewa mtoto.
Vuvuzela zimepigwa marufuku na vitu vingine kama maputo havitoruhusiwa. Taratibu hizi zitafuatwa katika mechi zote 64 zitakazochezwa Qatar.
0 Comments