Morocco waishangaza Dunia Qatar, waichapa Ubelgiji

Wawakilishi wa Bara la Afrika katika Michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar, Timu ya Morocco jana November 27 wameishangaza Dunia ya wapenda soka baada ya kuiadhibu Timu ya Ubelgiji mabao 2-0.



Mchezo huo wa kundi F uliacha maswali mengi kwa wapenda soka hasa kutokana na ubora wa Ubelgiji ambao wanakamata nafasi ya pili katika viwango vya ubora Duniani.


Magoli ya Morocco katika mchezo wa jana yamefungwa na Romain Saiss 73' na Zakaria Aboukhlal 90+2'.


Morocco wanajikusanyia alama 4 mpaka sasa baada ya mchezo wa kwanza kutoa sare na Croatia na mchezo unaofuata watakutana na Canada.


Croatia wanaongoza msimamao wa kundi F wakiwa na alama 4 baada ya kuichapa Canada mabao 4-1.


Ubelgiji watalazimika kupata ushindi mchezo wa mwisho dhidi ya Croatia ikiwa wanataka kufuzu kwa hatua ya 16 bora.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE