Brazil yaipiga Uswizi na kutinga 16 Bora

 Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Brazil imefuzu kucheza raundi ya kumi na sita (16) katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea Doha nchini Qatar baada ya kuilaza Switzerland goli moja nunge.



Wakongwe wa Brazil akiwemo Ronaldo de Lima walikaa kwa wasiwasi mwigi wakati wakifuatilia mchuano huo hasa baada ya kipindi tulivu cha kwanza.


Kipindi cha pili Brazil iliandika goli la kwanza dakika ya 67 hata hivyo furaha za mashabiki zilizimwa ghafla baada ya matokeo ya VAR kuonesha kulikuwa na kosa.


Bao la kustaajabisha la Casemiro dakika 10 kabla ya mpira kumalizika lilirejesha matumaini ya Brazil kusonga mbele. Na sasa Brazil imepanda ikiifuata Ufaransa ambayo iliishangaza Austaria kwa goli 4 - 1 siku ya Jumanne, na baadaye Denimika goli 2-1.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE