Game Supermarket kufunga maduka yake baada ya kukosa wateja Afrika Mashariki

Kampuni ya biashara za maduka kutoka Afrika Kusini Massmart, ambayo inaendesha Maduka ya Game, inapanga kufunga maduka yake Afrika Mashariki, baada ya maduka makubwa pinzani kupuuza ofa, na kutoa mwelekeo mpya wa matatizo yanayokabili biashara ya maduka makubwa katika eneo hilo.



Kampuni imesema imeshindwa kupata wanunuzi wa ndani wa maduka yake 14 ya Game nchini Kenya, Uganda, Tanzania, Ghana na Nigeria baada ya kuyaweka sokoni mwaka jana.


Kampuni hiyo imeanza mazungumzo na wafanyakazi wake kabla ya kufungwa rasmi kwa duka, kuashiria mwisho wa mapambano yake ya miaka saba kwenye soko na kuongeza kwenye orodha ya maduka yanayofunga biashara zake katika miaka ya hivi karibuni.


Chanzo : Jf

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE