Serikali yatangaza msako wanaowatumia walemavu kujipatia pesa

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Amon Mpanju amesema msako wa kuwakamata wale wote wanaowatumia walemavu ili kujipatia pesa utaanza hivi karibuni.



Ameyasema hayo katika kongamano la watu wenye ulemavu Wilaya ya Nyamagana lililoandaliwa na Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu nchini (Shivyawata) wilayani humo.


Amesema Serikali imegundua uwepo wa watu wanaofadhili ombaomba kwa maslahi yao (wafadhii) wenyewe, ambao wanawakusanya kutoka vijijini na kuwasafirisha hadi mijini kwa ajili ya kazi hiyo.


“Tumekutana wizara kadhaa kuweka miongozo itakayotuwezesha kulifanikisha hili. Tuko hatua za mwisho na utekelezaji utaanza muda wowote. Tunahitaji utu wa watu wenye ulemavu uwekwe mbele,” amesema.


Aidha, amewata watu wenye ulemavu kukubaliana na hali zao ili kutumia fursa za kiuchumi zilizopo, ikiwemo mikopo ya asilimia mbili inayotolewa na Halmashauri.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE