Changamoto za kipato zinafungua njia nyingi za kujiami lakini kuna njia zilizo sahihi na kuna njia ambazo sio sahihi. Mchezo au (upatu) sio njia rafiki inayoweza kuleta ahueni ya maisha.
Mchezo unakufanya kuwa mtumwa kiasi cha kuishi kwa wasiwasi ili kila siku utoe pesa ya watu.
Kuna watu wanajinyima hata kula yao kwasababu ya mchezo. Kuna watu wanauza mpaka thamani zao kwa ajili ya mchezo. Kuna watu wanaingia mpaka madeni ili kulipa mchezo. Sasa kitu chochote kinachokulazimu kiasi cha kukopa au kuiba hakishauriwi kufanywa katika uchumi.
Kujiwekea akiba wewe mwenye kutakupa uhuru wa kuweka na uhuru wa kutumia. Huwezi kukopa ili uweke akiba wala huwezi kuuza thamani zako ili uweke akiba. Utaweka akiba ukiwa huru na salama kile unachoweka.
Lakini upatu sio kitu salama kwasababu hata namna ya uwekaji wenu wa hela upo mkononi mwa mtu bila makubaliano ya kisheria yatakayokulinda endapo kama kunatokea mabadiliko.
Ushawahi kujiuliza siku kijumbe akifa nani atakupa hela yako?. Ushawahi kujiuliza kijumbe akikimbia na hela zako nani atakulipa?. Ni njia gani unaweza kujitetea endapo kijumbe atakapokataa kukupa jina lako ndani ya muda wako?.
Changamoto zote hizi unapojiwekea akiba wewe mwenyewe haziwezi kukufika. Kujiwekea fedha zako binafsi kuna kupa uhuru wa fedha mara kumi ya kucheza upatu.
0 Comments