Fahamu kila kitu kuhusu magari yanayotumia umeme kutoka Tesla

 

Tesla ni kampuni ya kiteknolojia inayounda na kutengeneza magari ya umeme pamoja na betri zake. Kampuni hii inatengeneza pia na vifaa maalum kwaajili ya kuvuna na kutunza umeme wa jua. Dhamira kuu ya kampuni hii ni kuharakisha ulimwengu kutumia nishati endelevu (Sustainable energy).


Kampuni ya Tesla ilianzishwa mwaka 2003 na kikundi cha mainjinia ambao walikuwa na hulka ya kutengeneza magari ya umeme yaliyo bora zaidi kuliko magari ya mafuta. Elon Musk aliwekeza katika kampuni hii tangu mwaka 2004 na kuwa Mkurugenzi mtendaji (CEO) mwaka 2008. Gari la kwanza kutengenezwa na kampuni hii lilikuwa ni Roadster  lililotengenezwa na kuanza kutumika mwaka 2008. Gari hii lilikuwa ndio gari la kwanza linalotumia umeme kufikisha umbali wa kilomita 394 kwa chaji ile ile iliyoanza nalo. Magari yaliyofuata kutengenezwa na kampuni hii ni.


Model S: Tesla iliyatengeneza magari haya ya Model S Sedan mwaka 2012. Magari haya yana uwezo wa kwenda mpaka kilomita 426 betri ikiwa imejaa chaji. Tesla Model S ni gari lililofanya mauzo makubwa katika kampuni ya tesla na kuipa sifa kampuni hiyo jambo ambalo lilipelekea watu kuwekeza zaidi katika kampuni hii.

Model X: Magari haya yalitengenezwa na Tesla mwaka 2015 na kuitwa Tesla Model X SUV. Gari hili lilikuwa ni kubwa kidogo kuliko Tesla Model S na pia lilikuwa na uwezo mkubwa zaidi. Gari ya Tesla Model X lina uwezo wa kwenda kilomita 580 ikiwa imejaa chaji.


Model 3: Tesla Model 3 Sedan lilitoka mwaka 2017 likiwa na sifa mbalimbali ikiwemo uwezo wa kujiendesha lenyewe pamoja na pia kufanyiwa maboresho ya mfumo kwa njia ya mtandao. Betri ikiwa imejaa gari hili lina uwezo wa kutembea mpaka kilomita 568 bila kuchajiwa. Kwa kipindi cha miaka mitatu gari hili limekuwa likishika nafasi ya kwanza kama gari lililouzika zaidi duniani.

Model Y: Mwaka 2020 Tesla walitengeneza gari ya Tesla Model Y Crossover ambayo ni ndogo kidogo kwa ile ya zamani Tesla MODEL X. Gari hili linatunza umeme wa kutembelea mpaka kilomita 525. Gari hili pia lina teknolojia ya kujiendesha lenyewe na linaweza kukimbia kuanzia 0 mpaka kilomita 97 ndani ya sekunde 5.3.


Magari ya Tesla yameleta mabadiliko makubwa katika ulimwengu wa teknolojia kwa kutumia umeme ambapo teknolojia hii inazidi kuendelezwa na kampuni hii kupitia matoleo mbalimbali ya magari haya. Endelea kutembelea tovuti yetu uweze kufahamu mambo mbalimbali kuhusu teknolojia. Soma makala zetu zingine hapa.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE