FRED LOWASA AWAHAIDI NEEMA WANANCHI WA MONDULI

……………………………………………………..
Na Woinde Shizza , Arusha
Mgombea ubunge wa Jimbo la Monduli Fred Lowasa ameaidi wananchi wake kuwa iwapo watampa ridhaa ya kuongoza Jimbo Hilo kwa kumpigia Kura za ndio kitu ambacho ataanza nacho Ni kutatua mgogoro wa wakulima na wafugaji uliopo monduli juu anaumaliza na kuakikisha vijiji 12 vilivyopo jimboni humo vinapata umeme.
Aliyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni katika Jimbo Hilo uliouthuriwa na   Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa   ambaye pia ni waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ambaye pia alipata wasaa wa kumuombea kura mgombea huyo pamoja na Rais John Magufuli
Alisema kuwa Jimbo la Monduli lina changamoto nyingi lakini changa Moto ya Kwanza ambayo akipita tu ataanza nayo kwa kuitatua ni Ile ya mgogoro uliodumu kwa mda mrefu baina ya wakulima na wafugaji
Alimshukuru waziri mkuu kwa kumuita aliekuwa mbunge wa Jimbo hilo  Julius Kalanga kumuombea kura na kubainisha kuwa kabla ya hapo walikuwa na wagombea wenzake 24 ambao waligombea Ila yeye ndio alishinda Mara baada ya kupigiwa Kura na  wajumbe na kuongoza wakampitisha lakini pia anashukuru vikao vya uteuzi vilimuona na vikaona anafaa na vikampitisha na pia anashukuru watia Nia wote kwani wamejitokeza kumuunga  mkono  na wameamua kusimama nae kwa ajili ya kukitafutia Kura Chama Cha mapinduzi
Aidha Alibainisha kuwa ahadi ambazo atazitoa katika siku za  kampeni atazitekeleza ,na alimuomba waziri  kuchukuwa Jambo la migogoro ya ardhi iliopo katika Wilaya ya Monduli maana Ni likubwa mno  na wafugaji na wakulima niwengi kutokana na watu kuongezeka huku alibainisha  binadamu wavyoongezeka  ndivyo maitaji ya ardhi yanavyoongezeka zaidi .
“Rais magufuli anauhusiano mzuri na Jimbo la Monduli iwapo mkimchagua mtapata neema kubwa sanasana na pia msisahau kuwapigia Kura madiwani wetu ,nathani mmeona nimekabidhiwa likitabu likubwa hapa nitaenda kukipitia ili niweze kujua vitu gani vilivyopo uko na nivifanyie kazi kwa kushirikiana na Chama changu na Serikali”alisema Fready
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ilani   ya Chama Cha mapinduzi Mgombea UbungeJimbo la Monduli, Fred Lowassa wakati alipozindua Kampeni za CCM wilayani Monduli
445 waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa akimuombea Kura mtoto wake Fred Lowasa wakati wa kampeni zilizofanyika katika uwanja was Barafu


source https://fullshangweblog.co.tz/2020/09/04/fred-lowasa-awahaidi-neema-wananchi-wa-monduli/

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE