Njia 6 za kutambua akaunti feki (parody) Twitter

Njia rahisi kabisa ya kutambua kama akaunti fulani inamilikiwa na mhusika ni kama mtandao husika umeithibitisha (verify) akaunti hiyo. Lakini uhalisia ni kwamba sio akaunti zote zinazothibitishwa, bali tu zile za watu mashuhuri, taasisi/kampuni au nchi fulani.

Kutokana na mtu mmoja kuwa na uwezo wa kutengeneza akaunti zaidi ya moja, kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kutengeneza akaunti kwa kutumia taarifa za watu wengine, au za kubuni kwa sababu wanazozijua wao.

Lakini je! Kwa namna gani unaweza kutambua akaunti fulani ni bandia (parody)? Si rahisi sana kuweza kujua kwa sababu baadhi ya watu huwa makini wakati wa kuunda akaunti hizo. Kwa ujumla, haya ni mambo yanayoweza kukupa ishara kuwa akaunti husika ni bandia;

Ilitengenezwa lini?
Mara nyingi akaunti bandia hutengenezwa muda mfupi baada ya tukio fulani kutokea. Ukiona jambo fulani lina trend, na ghafla ukaona akaunti kuhusu jambo au mtu hiyo, tilia mashaka uhalali wake.

Matumizi ya picha
Parody nyingi hupenda kutumia picha za wasichana warembo sana kwa sababu lengo ni kuwavutia wafuasi wengi zaidi.

Tweets
Kwa wastani mtumiaji wa kawaida wa Twitter anaandika jumbe 10 hadi 15 kwa siku. Lakini Parody kwa sababu imetengenezwa kwa sababu maalum hu-tweet mara nyingi zaidi, hadi mara 500 kwa siku.

Kuficha taarifa
Angalia kwenye picha anayotumia, angalia handle yake, angalia taarifa za akaunti pamoja na Bio yake. Vyote hivi vitakupa ishara kwa sababu akaunti feki huwa na taarifa ambazo zinatia mashaka au haziwekwi taarifa kabisa. Handle huwa na namba namba ambazo hazieleweki, picha inaweza kuwa yai au mazingira. Kadiri taarifa zinavyokuwa chache, ni dalili kuwa ni parody.

Jumbe
Mara nyingi akaunti ambazo ni parody, kwa sababu zimetengenezwa kwa lengo fulani, hujikita katika jambo hilo bila kuzungumzia mambo mengine. Pia, hu-retweet zaidi kuliko hata zinavyoandika tweets zao wenyewe.

Wafuasi
Mara nyingi akaunti hizi huwafuata watu wengi zaidi kuliko wanaowafuta. Kwa sababu wanataka idadi kubwa ya wafuasi, hivyo hufuata watu wengi, kwa imani kuwa nao watawafuata, ili ujumbe wake ufike kwa wengi zaidi.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE